Yanga - Local

Ni fainali ya kihistoria kwa Yanga

Joel JJ By Joel JJ
β€’
28 May 2023
Ni fainali ya kihistoria kwa Yanga

Jioni ya leo macho na masikio ya Watanzania yataelekezwa uwanja wa Benjamin Mkapa kuwashuhudia Wananchi wakicheza fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya USM Alger

Ni mchezo wa mkondo wa kwanza ambao utapigwa saa 10 jioni wakati fainali ya pili itapigwa Algeria Ijumaa ijayo

Ni mechi ya kihistoria kwa Yanga na Tanzania kwa sababu hii ni mara ya kwanza mechi ya fainali ya michuano ya CAF inapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa

Mwaka 1993 Simba walicheza fainali ya kombe la Washindi Afrika mchezo dhidi ya Stella Abidjan ukipigwa uwanja wa Uhuru (Shamba la Bibi) hivyo leo historia itaandikwa dimba la Mkapa kwa mechi ya fainali ya kombe la Shirikisho (CAF CC) kupigwa katika uwanja huo

Nafasi nadra kwa mashabiki kushuhudia mtanange huo wa kihistoria, ni wazi siti zote 60,000 zitakuwa na watu kwani tiketi zote za mchezo huo zimeuzwa

Yanga inawania taji kubwa la kwanza barani Afrika, leo inahitaji kushinda ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kumaliza kazi ugenini kwenye mchezo wa pili

Yanga imepata maandalizi mazuri, kocha Nasreddine Nabi, wachezaji wamezungumza jinsi walivyo tayari kwa mchezo huo

Sapoti ya mashabiki hakuna shaka itakuwa kubwa lakini muhimu Wananchi wanapaswa kushangilia kwa muda wote wa mchezo ili kuhakikisha morali ya wachezaji wao haishuki

Wachezaji wa Yanga wanahitaji kufunga bao mapema ili kuvuruga mbinu za wapinzani wao ambao inafahamika mbinu watakayotumia zaidi leo ni kucheza kwa tahadhari pamoja na kupoteza muda

Mipira ya adhabu na kona inapaswa kudhibitiwa vyema kwani hiyo ndio itakuwa silaha kubwa ya USM Alger katika mchezo huo pamoja na kocha wao kudai hawakuja Tanzania kupaki basi

Hii ni siku ya kihistoria kwa Yanga na nchi kwa ujumla, matumaini ni kuona Yanga ikiibuka na ushindi mnono leo

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
4h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
4h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
4h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
8h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
11h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
12h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
12h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
13h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
14h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
15h ago
READ MORE β†’