Transfer - International

Tetesi za soka Ulaya, Jumatatu, May 29 2023

Joel JJ By Joel JJ
β€’
29 May 2023
Tetesi za soka Ulaya, Jumatatu, May 29 2023

Barcelona wanataka kumsajili kiungo wa kati wa Brazil Bruno Guimaraes, lakini klabu hiyo inaamini itapaswa kutoa ada ya uhamisho ya takriban euro milioni 100 (£87m) ili kuwashawishi Newcastle United kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25. (Times)

Real Madrid wanafikiria kumnunua mshambuliaji wa Brazil Roberto Firmino, 31, ambaye atakuwa mchezaji huru mkataba wake na Liverpool utakapokamilika msimu huu wa joto. (Fabrizio Romano)

Meneja wa zamani wa Tottenham na Paris St-Germain Mauricio Pochettino, 51, ametia saini mkataba wa miaka mitatu kuwa kocha mkuu mpya wa Chelsea. (Guardian)

Brazil bado wana matumaini ya kumshawishi kocha wa Real Madrid Carlo Ancelotti kuwa kocha wao mkuu ajaye. Mabingwa hao mara tano wa dunia wamekuwa bila kocha tangu Tite alipoondoka mara baada ya fainali za Kombe la Dunia huko Qatar mwezi Disemba. (Athletic)

Liverpool wanaweza kumsajili kiungo wa Lazio Sergej Milinkovic-Savic, 28, kwa euro 26m (£22.5m), huku mkataba wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Serbia ukitarajia kumalizika 2024. (Calciomercato via Goal)

Matumaini ya Manchester United kumsajili beki wa Korea Kusini Kim Min-jae, 26, na mshambuliaji wa Nigeria Victor Osimhen, 24, kutoka Napoli yameongezeka huku kukiwa na uvumi kuhusu mustakabali wa meneja wa timu hiyo ya Italia Luciano Spalletti. (Givemesport)

Newcastle United pia wameingia kwenye kinyang'anyiro cha kutaka kumsajili Kim wa Napoli. (Fijaches)

Sheffield United inamfuatilia kiungo wa kati wa Nottingham Forest Muingereza Lewis O'Brien, 24, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo DC United. (Sun)

Crystal Palace wanakaribia kufikia makubaliano ya kumsajili kiungo wa kati wa Bournemouth na Colombia Jefferson Lerma, 28, kwa uhamisho huru (wa bure) msimu huu wa joto. (Fabrizio Romano)

Mshambuliaji na mchezaji aliye huru wa Chile Alexis Sanchez, 34, anatamani tena kurejea katika Ligi kuu ya England - baada ya kuzichezea Arsenal na Manchester United – wakati huu akimaliza mkataba wake Marseille. (Sun)

BBC

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
9h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
10h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
10h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
14h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
17h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
18h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
18h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
19h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
20h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
20h ago
READ MORE β†’