Ligi Kuu Uingereza ilivyohitimishwa

Joel JJ By Joel JJ β€’ 29th May 2023


Ligi Kuu Uingereza ilivyohitimishwa

Pazia la Ligi kuu England limefungwa rasmi jana Mei 28, 2023 huku Leicester City na Leeds United zikiungana na Southampton kushuka daraja kwenda Ligi ya Championship 

Klabu ya Everton imenusurika kushuka daraja kufuatia ushindi wa 1-0 dhidi ya Bournemouth huku Chelsea ikimaliza ikiwa nafasi ya 12 kwenye msimamo wa Ligi

Bingwa ni Manchester City huku Arsenal, Man United na Newcastle United zikimaliza katika nafasi ya pili, tatu na nne

Liverpool na Brighton zitacheza Europa League msimu ujao huku Aston Villa ikiambulia nafasi ya kucheza UEFA Conference League

Erling Haaland ameshinda tuzo mchezaji bora wa Ligi Kuu ya 2022/2023 huku pia akishinda tuzo ya PFA


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.