Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Dk Fredrick Shoo amesema ni wakati wa kuweka ushabiki pembeni na kuiombea Yanga, ili kuweza kutwaa ubingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika
Dk Shoo ambaye pia ni Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) alitoa rai hiyo wakati akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya CCT, ambapo yalifanyika kitaifa katika Usharika wa Moshi mjini mkoani Kilimanjaro na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa dini na serikali, akiwemo Waziri wa Fedha, Dk Mwigulu Nchemba ambaye alikuwa mgeni rasmi
Dk Shoo amesema Yanga inaiwakilisha nchi ya Tanzania katika Kombe la Shirikisho Afrika, hivyo watanzania wote wanapaswa kuweka ushabiki wa ndani pembeni na kuiombea pamoja na kuitia moyo, ili waweze kufanikiwa kuutwaa ubingwa
Yanga ilipoteza mchezo wa mkondo wa kwanza wa fainali kwa kufungwa mabao 2-1 dhidi ya USM Alger timu hizo zikitarajiwa kurudia nchini Algeria Jumamosi, Julai 03