Licha ya tetesi kumuhusisha na miamba ya soka Afrika Kusini, Kaizer Chiefs, mlinzi wa Simba na timu ya Taifa Mohammed Hussein 'Zimbwe Jr' anatarajiwa kusaini mkataba mpya kuendelea kubaki Msimbazi
Chanzo cha uhakika kutoka ndani ya uongozi wa Simba kimethibitisha kuwa Zimbwe Jr amefikia makubaliano na Simba ili kusaini mkataba mnono ambao utamfanya aendelee kubaki Msimbazi kwa misimu mingine miwili
Hata hivyo haikuwa rahisi kumshawishi Zimbwe Jr kusalia kwani Chiefs waliweka mezani ofa nono ambayo sio rahisi kukataa
Simba pia inaendelea na mazungumzo na mlinzi wa kulia Shomari Kapombe ambaye pia anatarajiwa kusaini mkataba mpya
Simba imedhamiria kuwabakisha wachezaji wake wote muhimu na kusajili wachezaji bora zaidi kwenye nafasi zilizoonekana kuwa na changamoto



