Kiungo wa Yanga, Feisal Salum 'Feitoto' amesema hana tatizo lolote na klabu ya Yanga ila ana tatizo na Rais wa klabu hiyo, Mhandisi Hersi Said
Akizungumzia sakati lake na mabingwa hao wa Tanzania Bara katika mahojiano ya Clouds FM radio, Feisal aliweka wazi kuwa yuko tayari kurejea Yanga iwapo kama Hersi ataondoka
"Kuna tofauti kubwa mno kati ya kiongozi wa juu wa Yanga aliyepita na huyu aliyepo hivi sasa. Hersi akiondoka Yanga ninafunga vitu vyangu haraka na kurudi kwenye kambi ya Yanga," alisema Feisal
Feisal ameusifu uongozi wa Dk Mshindo Msolla kuwa ulikuwa bora na kusikiliza wachezaji kuliko wakati huu ambao timu hiyo iko chini ya Rais Hersi
Hata hivyo kauli hiyo ya Feisal ni kama inakinzana na madai yake ya kuvunja mkataba kuwa sababu ilikuwa ni maslahi madogo aliyokuwa akilipwa na Yanga
Imebainisha kuwa mvutano uliopo kati yake na Yanga unatokana na sintofahamu iliyopo kati yake ya Rais wa Yanga Injinia Hersi Said



