Manula afanyiwa upasuaji Afrika Kusini

Joel JJ By Joel JJ β€’ 1st June 2023


Manula afanyiwa upasuaji Afrika Kusini

Mlinda lango wa Simba Aishi Manula amekamilisha matibabu Afrika Kusini akitarajiwa kurejea nchini baada ya afya yake kuimarika

Manula alifanyiwa upasuaji siku ya Jumanne katika Hospitali moja katika jiji la Johanesburg

Daktari wa Simba Edwin Kagabo ambaye aliongozana na Manula huko Afrika Kusini, amesema upasuaji ulikwenda salama na siku ya Ijumaa wataruhusiwa kutoka Hospitalini

Hata hivyo Kagabo amesema bado hawajafahamu Manula atakuwa nje kwa muda gani kutokana na aina ya matibabu aliyofanyiwa

Manula alichanika nyama za paja katika mchezo wa robo fainali kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) dhidi ya Ihefu Fc uliopigwa April 7


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.