Simba yamtema Okrah

Joel JJ By Joel JJ β€’ 5th June 2023


Simba yamtema Okrah

Uongozi wa klabu ya Simba umetangaza kuachana na kiungo mshambuliaji Augustine Okrah baada ya kumalizika Msimu wa mashindano wa 2022/23

Okrah raia wa Ghana amemaliza mkataba wake Wekundu wa Msimbazi na uongozi umeamua kutohuisha mkataba wake

Okrah alijiunga na Simba akitokea Benchem United ya Ghana ambapo ameonyesha uwezo mkubwa katika mechi zote alizocheza

Katika msimu mmoja aliohudumu ndani ya Simba Okrah amekuwa na mchango mkubwa akicheza mechi 17 na kufunga mabao manne na kusaidia kupatikana kwa jingine moja

Simba imeanza mchakato wa maboresho ya kikosi chao kuelekea msimu wa mashindano 2023/24


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.