Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan leo Juni 05, 2023 ameialika timu ya Yanga kupata chakula cha jioni Ikulu, Dar es Salaam ikiwa ni pongezi kwa kufanya vizuri katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika
Rais wa Yanga Injinia Hersi Said amesema timu nzima itahudhuria mwaliko huo kabla ya kuelekea mkoani Mbeya wanakokabiliwa na mechi mbili za ligi kuu dhidi ya Mbeya City na Tanzania Prisons
Hersi amesema Yanga ilipaswa kuondoka Dar es salaam leo saa 1 usiku kuelekea Mbeya lakini sasa wataondoka baada ya kuhudhuria mwaliko wa Rais Samia ambaye pia ametoa ndege kuwapeleka mkoani Mbeya
Rais Samia amekuwa chachu ya mafanikio kwa klabu za Yanga na Simba msimu huu kwenye mashindano ya CAF akitoa bonus ya fedha kwa kila hatua ambayo kila timu ilifikia
Wakati Simba ilitolewa hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa barani Afrika, Yanga imefanikiwa kutinga fainali na kukosa ubingwa kwa mujibu wa kanuni tu baada ya sare ya mabao 2-2 dhidi ya USM Alger