Ligi Kuu ya NBC inafika tamati wiki hii ambapo leo mechi zote za raundi ya 29 zitapigwa katika viwanja mbalimbali
Mabingwa wateule, Yanga wao wako mkoani Mbeya kuikabili Mbeya City katika mechi ya kukamilisha ratiba kwa upande wao huku Mbeya City wakihitaji kushinda ili kujihakikishia usalama wa kubaki ligi kuu
Simba itakuwa uwanja wa Azam Complex kumenyana na Polisi Tanzania katika mchezo utakaopigwa saa 1 usiku
Kwa Simba ni mchezo wa kukamilisha ratiba tu wakati Polisi Tanzania wanahitaji ushindi ili kuendelea kuweka hai matumaini madogo ya kubaki ligi ambapo pia hatma yao itategemea na matokeo ya timu nyingine

ADVERTISE HERE