Rais Samia atoa maagizo kwa Yanga sakata la Fei Toto

Joel JJ By Joel JJ β€’ 6th June 2023


Rais Samia atoa maagizo kwa Yanga sakata la Fei Toto

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan ameitaka Klabu ya Yanga kumaliza mgogoro na kiungo Feisal Salum ' Fei Toto'

Rais Samia ametoa agizo hilo jana June 5, 2023 katika hafla ya chakula ya jioni ya kuwapongeza Yanga kwa kushiriki fainali za michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika 

Rais Samia amesema amesema hafurahishwi na migogoro kati ya viongozi na wachezaji, hivyo amewaagiza viongozi wa Yanga wakaumalize mgogoro wa Fei Toto

"Haipendezi klabu kubwa kama hii kuwa na ugomvi na mtoto mdogo, hebu kamalizeni, kisha mje nyumbani kunieleza," alisema

Yanga wamekuwa na mgogoro wa kimkataba wa muda mrefu na kiungo huyo huku Kamati ya Sheria na Hadhi ya wachezaji ambayo ilisikiliza malalamiko ya pande zote na kuamua kuwa mchezaji huyo bado anamkataba na Yanga mpaka 2024

Fei aliondoka Yanga kuanzia mwishoni mwa mwaka jana, baada ya kudai kuwa anahitaji maslahi zaidi, akavunja mkataba kwa kuweka kiasi cha Sh milioni 112 kwenye akaunti ya klabu hiyo, lakini baadaye Kamati ya Sheria Hadhi za Wachezaji iliyopo chini ya Shirikisho la Soka Tanzania TFF, ilisema kuwa mchezaji huyo bado ni mali ya Yanga kwa kuwa hakufuata taratibu za kuvunja mkataba huo


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.