Aston Villa wameingia kwenye kinyang'anyiro cha kumsajili mchezaji huru Youri Tielemans, 26, baada ya kiungo huyo wa Ubelgiji kuondoka Leicester. (Athletic)
Chelsea imeungana na Barcelona na Liverpool katika mbio za kuwania saini ya kiungo wa Celta Vigo ya Uhispania Gabri Veiga. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 ana kifungu cha kuachiliwa cha pauni milioni 34.4. (Guardian)
Tottenham Hotspur wameonyesha nia ya kumnunua mlinzi wa Manchester United na England Harry Maguire, 30, na wanatumai kuwa wanaweza kumshawishi mchezaji mwenzake wa kimataifa Harry Kane kusalia katika klabu hiyo. (Telegraph, usajili unahitajika)
United wanataka kuwauza wachezaji wanane msimu huu - nahodha Maguire, mshambuliaji Anthony Martial 27, viungo Fred, 30, na Scott McTominay, 26, kipa Dean Henderson, 26, na mabeki Alex Telles, 30, Eric Bailly, 29, na Brandon Williams, 22. (Mirror)
Mshambulizi wa Crystal Palace na Ivory Coast ambaye kandarasi imeisha Wilfried Zaha, 30, amepokea ofa ya pauni milioni 15 kwa mwaka ili kuungana na Cristiano Ronaldo katika klabu ya Al-Nassr ya Saudi Arabia. Atletico Madrid pia wanavutiwa na mchezaji huyo. (Sky Sports)
Kiungo wa Chelsea na Ufaransa N'Golo Kante, 32, anapewa mshahara ambao unaweza kufikia £86.2m kwa mwaka na klabu za Saudi Al-Ittihad na Al-Nassr. (Guardian)
Mazungumzo kati ya Arsenal na wawakilishi wa beki wa Ufaransa William Saliba, 22, kuhusu mkataba mpya yanaendelea vyema. (Football London)
Mshambulizi wa Lille na Marekani Timothy Weah, 23, anaweza kuwa karibu na uhamisho wa pauni milioni 8.6 kwenda Juventus. (Goal)
Brighton wanatathmini dau lililoboreshwa la pauni milioni 40 kumnunua mlinzi wa Chelsea mwenye umri wa miaka 20 Levi Colwill. (Mail)
BBC