Mabao matano ya kiungo mshambuliaji wa Simba Saido Ntibazonkiza aliyoyafunga Juni 6, 2023, dhidi ya Polisi Tanzania katika michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara, yamechochea mbio za kuwania tuzo za ufungaji bora, akiwa nyuma ya bao moja kwa kinara Fiston Mayele
Mayele na Saido kwa pamoja wamekuwa na msimu bora hadi sasa ligi ikielekea ukingoni, mbali na mbio za ufungaji bora lakini kwa pamoja pia wanawania tuzo ya mchezaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara

Ilhali Saido, anawania pia tuzo ya kiungo bora wa ligi hiyo msimu huu, ambapo hadi kufikia mzunguko wa 29 ikiwa kila timu imesaliwa na mchezo mmoja tu
Saido amehusika katika jumla ya mabao 27, akifunga 15 na kutoa pasi za mabao 12 wakati Mayele amehusika katika mabao 19, akifunga 16 na kutoa assist tatu
Mchezo wa mwisho siku ya Ijumaa Simba itahitimisha na Coastal Union uwanja wa Uhuru wakati Yanga itahitimisha na Tanzania Prisons uwanja wa Sokoine Mbeya



