Baada ya Yanga kuthibitisha kumuuza kiungo Feisal Salum kwenda klabu ya Azam Fc, mchezaji huyo kutoka visiwani Zanzibar ametambulishwa rasmi na Azam FC
Feisal anakuwa usajili wa kwanza kufanywa na Azam Fc kuelekea msimu ujao wa mashindano 2023/24
Baada ya kusaini mkataba wa kuitumia Azam FC, Feisal amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumaliza sakata lake la kuvunja mkataba na klabu ya Yanga
Katika hatua za mwisho Feisal aliomba kuchangiwa fedha kwenda Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) kwa ajili ya suala la kimkataba na fedha hizo zilifikia Sh9 milioni
"Pesa sijui nani alitoa na nani ambaye hajatoa, kwahiyo mimi ambacho nitakifanya nitapeleka kwa watoto yatima, msikitini na nyingine kanisani, siwezi kurudisha nitapeleka kwa watu wenye uhitaji," alisema Feisal