Ligi Kuu ya NBC imefikia tamati leo kwa Yanga kukabidhiwa kombe baada ya mchezo dhidi ya Tanzania Prisons ambao ulimalizika kwa Yanga kushinda mabao 2-0
Kiungo mshambuliaji wa Simba Saido Ntibazonkiza amefungana na Fistom Mayele kwa mabao baada ya wote kufunga mabao 17
Saido ameifungia mabao mawili Simba leo katika mchezo dhidi ya Coastal Union Simba ikishinda mabao 3-1
Mayele alifunga bao moja na kutoa assist moja katika ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Prisons
Licha ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mbeya City, timu hizo zitacheza play-off kuwania kusalia ligi kuu baada ya kumaliza katika nafasi ya 14 na 13
Azam Fc imeifumua Polisi Tanzania mabao 8-0 Prince Dube akifunga mabao manne katika mchezo huo uliopigwa uwanja wa Azam Complex
Polisi Tanzania na Ruvu Shooting tayari zilishashuka daraja kabla ya mechi za mwisho leo



