Klabu ya Yanga leo Jumamosi kuanzia saa 5 asubuhi itasherehekea ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC waliotwaa kwa msimu wa pili mfululizo kwa kufanya Parade kutoka uwanja wa Ndee wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere hadi Makao Makuu ya klabu hiyo, Jangwani
Kulingana na ratiba iliyotolewa na Yanga, kikosi cha Yanga kitawasili jijini Dar es salaam wakitokea Mbeya majira ya saa 5 asubuhi na kubebwa na gari maalum la wazi
