Manchester City imetwaa taji la kwanza la Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Inter Milan ya Italia usiku wa Jumamosi katika Uwanja wa Ataturk Olynmpiya huko Uturuki
Bao pekee la Manchester City lilifungwa na kiungo wa Kimataifa wa Hispania, Rodri dakika ya 68
Licha ya Manchester City kutawala kwa muda mwingi, ulikuwa mchezo wa nafasi chache Inter Milan wakiwa imara katika kujilinda
Kama sio umahiri wa mlinda lango wa Manchester City Ederson, Inter Milan wangeweza kurejesha bao hilo kwenye dakika za majeruhi Inter wakifanya mashambulizi makali langoni kwa Man City
Manchester City imefikia rekodi ya kushinda mataji matatu katika msimu mmoja, rekodi iliyowekwa na mahasimu wao Manchester United mwaka 1999
Linakuwa taji la kwanza kwa kocha Pep Guardiola kushinda tangu alipoondoka FC Barcelona, likiwa ni taji lake la tatu la Ligi ya Mabingwa



