Al Ahly ya Misri imefanikiwa kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Afrika licha ya sare ya 1-1 dhidi ya wenyeji Wydad Athletic Club waliokuwa pia wanashikilia taji hilo usiku wa jana Uwanja wa Mohamed V Jijini Casablanca nchini Morocco
Wydad walitangulia na bao la beki wake, Yahya Attiat-Allah El Idrissi dakika ya 27, kabla ya Mohamed Abdelmonem kuisawazishia Al Ahly dakika ya 78
Al Ahly wanabeba Kombe kwa ushindi wa jumla wa 3-2, kufuatia kuwachapa Wydad 2-1 kwenye mchezo wa kwanza wiki iliyopita Jijini Cairo na hilo linakuwa taji la 12 jumla kwao wakiendelea kuwa washindi wa mataji hayo mengi zaidi
Al Ahly hawakuanza vyema msimu wa ligi ya mabingwa wakilazimika kutinga robo fainali kwa uwiano wa mabao mbele ya Al Hilal
Lakini imekuwa kawaida yao wanapofika robo fainali timu hubadilika