Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) limerejea tena kwenye makabati ya Yanga pale Jangwani baada ya kuichapa Azam Fc bao 1-0 katika mchezo wa fainali uliopigwa uwanja wa Mkwakwani
Alikuwa ni Kennedy Musonda aliyeihakikishia Yanga medali ya dhahabu ya tatu msimu huu akifunga bao pekee kwa kichwa kwenye dakika ya 13
Haikuwa mechi rahisi timu hizo zikigawana vipindi, Yanga ikiwa bora katika kipindi cha kwanza na Azam Fc wakiwa bora katika kipindi cha pili
Ni msimu wa pili mfululizo Yanga inashinda mataji yote ya ndani kuanzia Ngao ya Jamii, Ligi Kuu na leo kombe la Shirikisho la Azam (ASFC)
Kwa hakika huu unaweza kuwa msimu bora zaidi kwa Yanga katika historia yao wakiwa pia wamecheza fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika (CAF CC)

