Manchester United itaongoza kinyang'anyiro cha kumnunua fowadi wa Ufaransa Kylian Mbappe, 24, kutoka Paris St-Germain ikiwa klabu hiyo ya Ligi Kuu ya Uingereza itanunuliwa na Sheikh Jassim bin Hamad Al Thani. (Metro)
Chelsea pia wanatarajiwa kumtaka Mbappe baada ya mshambuliaji huyo kuwaambia PSG kuwa hataki kuongeza mkataba wake nao zaidi ya 2024. (Times – Subscription Required).
Real Madrid pia wanataka kumsajili Mbappe msimu huu wa joto, jambo ambalo litaboresha uwezekano wa Tottenham kumbakisha mshambuliaji wa Uingereza Harry Kane, 29, ambaye pia amekuwa akihusishwa na klabu hiyo ya Uhispania. (Mail)
Hata hivyo, wawakilishi wa Kane pia wamekutana na viongozi wa PSG. (Mirror)
Manchester United wako tayari kumuuza winga wa England Jadon Sancho, lakini wakati Aston Villa wanamtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23, hawataki kulipa bei inayotakiwa ya pauni milioni 60. (Football Transfers)
Arsenal hawana mpango wa kumrejesha tena mchezaji aliyevunja rekodi ya klabu kwa pauni milioni 72 Nicolas Pepe katika kikosi chao na wanataka kumuuza mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast mwenye umri wa miaka 28 msimu huu. (Telegraph – Subscription Required)
Mshambulizi wa Chelsea na Ubelgiji Romelu Lukaku, 30, amepewa ofa ya pauni milioni 20 kwa msimu na klabu ya Al-Hilal ya Saudi Arabia. (Guardian)
Aston Villa na Wolverhampton Wanderers wanavutiwa na kiungo wa kati wa Borussia Monchengladbach Mfaransa Manu Kone, 22, ambaye pia amekuwa akihusishwa na Liverpool. (Mail)
Tottenham wanakaribia kuafikiana na kipa wa Brentford David Raya, 27, na wanatumai kujadili ada ya chini na The Bees, ambao wanataka pauni milioni 40 kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Uhispania. (Standard)
Beki wa Barcelona na Uhispania Jordi Alba, 34, yuko kwenye mazungumzo na Inter Miami kuhusu kuhamia Ligi Kuu ya Soka. (Fabrizio Romano)
Barca wanamfuatilia kiungo wa kati wa Villarreal Mhispania Alex Baena, 21, kama mbadala wa kiungo wa kati wa Manchester City na Ujerumani Ilkay Gundogan, 32. (ESPN)
Coventry City wanavutiwa na beki wa Chelsea mwenye umri wa miaka 20 Muingereza Bashir Humphreys. (Standard)
BBC