Baada ya kukamilisha usajili wao wa kwanza msimu huu wakimn'goa Feisal Salum 'Fei Toto' kutoka klabu ya Yanga, matajiri wa Azam Fc jana walitangaza kuachana na makocha wawili na wachezaji watatu
Kocha wa magolikipa Dani Cadena na kocha wa viungo Dk Moadh Hiraoui wamepewa mkono wa kwa heri
Timu hiyo pia imetangaza pia kuachana na nyota wao Bruce Kangwa raia wa Zimbabwe aliyedumu kikosini hapo kwa misimu Saba
Kangwa alikuwa nahodha wa timu hiyo alijiunga na Azam Fc mwaka 2016 akitokea Highlanders ya Zimbabwe
Azam Fc pia imeachana na kiungo wa kimataifa wa Kenya Kenneth Muguna pamoja na Mshambuliaji kutoka Zambia Rodgers Kola