Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amesema mchakato wa kusaka kocha mpya umeanza na tayari wamepokea CV nyingi za makocha
Kamwe amesema uongozi wa Yanga utaendesha mchakato wa kusaka kocha mpya kwa weledi na umakini ili kuhakikisha Kocha atakayekuja ataendeleza mazuri yalioachwa na Nasreddine Nabi
"Baada ya kutangaza kuondoka kwa kocha Nabi, katika saa 24 zilizopita tumepokea zaidi ya CV 1000 za makocha wanaotaka kuja kuifundisha timu yetu"
"Niwaambie wapenzi na wanachama wetu kuwa uongozi wao uko makini na wataleta kocha mwenye viwango ambaye ataweza kutimiza malengo ya klabu"
"Tunaheshimu uamuzi wa Kocha Nabi ambaye tulipenda kuendelea nae lakini ameona ni wakati sahihi kwake kwenda kutafuta changamoto mahali pengine baada ya mafanikio aliyotupa katika misimu miwili iliyopita," alisema Kamwe
Nabi anatarajiwa kujiunga na klabu ya Kaizer Chiefs baada ya misimu miwili na nusu na mafanikio katika klabu ya Yanga