Azam - Local

Miaka 14 ya Morris na Azam Fc imehitimishwa

Joel JJ By Joel JJ
β€’
17 Jun 2023
Miaka 14 ya Morris na Azam Fc imehitimishwa

Matajiri wa Chamazi Azam FC wametangaza kufikia ukomo na Kocha wake msaidizi Agrey Moris Ambros aliyehudumu klabuni hapo tangu 2009 akiwa mchezaji kijana, nahodha na pia sehemu ya benchi la ufundi

Taarifa hiyo imetolewa leo Juni 17, 2023 kupitia akaunti rasmi ya Instagram ya Klabu hiyo huku ikitoa shukurani kwa Ambros kwa muda wote aliyehudumu klabuni humo.

"Daima utabakia kwenye historia ya klabu yetu. Tunakutakia kila la kheri kwenye maisha yako mapya. You area a truelegend Agrey Moris Ambros"

Itakumbukwa mwanzoni mwa Juma Azam walitangaza kuachana na wachezaji kama nahodha Bruce Kangwa, Rogers Kolla, Ismail Aziz Kader, Daniel Amoah sambamba na Kocha wa walinda lango Dani Cadena bila kusahau aliyekuwa Kaimu Kocha Mkuu wa klabu hiyo Kalimangonga Ongala

Huu ni muendelezo wa panga pangua ya safu ya Azam FC na vilabu vingine nchini ikiwa ni maandalizi ya msimu ujao 2023/24 ambapo msimu uliotamatika Azam FC walimaliza wakiwa nafasi ya tatu huku wakikusanya alama 59 katika michezo 30 ya NBCPL sambamba na kumaliza nafasi ya pili ya Kombe la Shirikisho Azam baada ya kufungwa 1-0 katika mchezo wa fainali dhidi ya Yanga.

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
9h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
10h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
10h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
14h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
17h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
18h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
18h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
19h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
20h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
20h ago
READ MORE β†’