Kiungo kiraka wa Yanga Yannick Bangala amesema ataendelea kubaki katika kikosi cha Yanga kuhudumia mkataba wake
Siku chache zilizopita Bangala alitoa kauli yenye utata akidai ana asilimia 20 ya kubaki ndani ya kikosi cha Yanga msimu ujao
Lakini kulingana na mahojiano aliyofanya na Manara TV, Bangala amesema ataendelea kutumikia mkataba wake wa mwaka mmoja katika kikosi cha Yanga
"Mimi naipenda Tanzania, nafurahi kucheza hapa, bado nina mkataba na Yanga hivyo niteendelea kubaki hapa," alisema
Tangu sakata la Feisal Salum, uongozi wa Yanga umeweka msimamo kwa mchezaji yeyote anayetaka kuondoka wakati mkataba wake ukiwa haujamalizika ni lazima afuate utaratibu kwa kufanya mazungumzo na mabosi wake au kuitaarifu timu inayomtaka iwasilishe ofa Jangwani
Bangala na mlinzi wa kulia Juma Shaban msimu uliopita walisaini mkataba wa miaka miwili kila mmoja, mikataba ambayo itawaweka Jangwani mpaka mwishoni mwa msimu wa 2023/24



