Klabu ya Yanga jana ilithibitisha kuahana na kiungo mshambuliaji Dickson Ambundo ambaye amemaliza mkataba
Ambundo alijiunga na Yanga misimu miwili nyuma akitokea klabu ya Dodoma Jiji
Taarifa za kuaminika kutoka mkoani Dodoma zimebainisha kuwa nyota huyo wa zamani wa klabu za Alliance Fc na Gor Mahia ya Kenya, anarejea kwa waajiri wake wa zamani, Dodoma Jiji
Katika misimu miwili aliyocheza Yanga, Ambundo amefanikiwa kushinda mataji sita pamoja na kuishuhudia timu yake ikicheza fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika