Tetesi za soka Ulaya, Jumatano Juni 21 2023

Joel JJ By Joel JJ β€’ 21st June 2023


Tetesi za soka Ulaya, Jumatano Juni 21 2023

Fulham wanataka kumsajili kiungo wa Brazil Fred, 30, anayechezea klabu ya Manchester United. (Telegraph - usajili unahitajika)

Everton wana nia ya kumnunua kipa wa Crystal Palace na Uingereza Sam Johnstone, 30, ikiwa Jordan Pickford ataondoka katika klabu hiyo. (Sun)

Leicester City wanataka zaidi ya pauni milioni 50 kumnunua kiungo wa Uingereza James Maddison, 26, huku Tottenham na Newcastle zikimwania. (Sky Sports)

Manchester City wanakaribia kuafikiana kibinafsi na beki wa RB Leipzig wa Croatia Josko Gvardiol, 21. (Fabrizio Romano)

Arsenal wametoa ofa iliyoboreshwa ya £60m kwa mshambuliaji wa Chelsea na Ujerumani Kai Havertz, 24. (Mail)

Newcastle wanafikiria kusitisha nia yao ya kumnunua kiungo wa kati wa Inter Milan na Italia Nicolo Barella, 26. (Independent)

Crystal Palace wanamtaka Roy Hodgson mwenye umri wa miaka 75 kusalia kama mkufunzi. (Guardian)

Lakini Newcastle inapania kumsajili mshambuliaji wa Ujerumani Derry Scherhant, 20, kutoka Hertha Berlin. (Telegraph - usajili unahitajika)

Manchester City, Chelsea na Liverpool wanawania kumsajili kiungo wa kati wa Real Madrid na Uruguay Fede Valverde, 24, msimu huu. (Teamtalk)

BBC


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.