Ligi Kuu ya Vijana U20 imeanza kutimua vumbi leo katika uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar es salaam
Michuano hiyo inahusisha timu za vijana za klabu zilizoshiriki ligi kuu ya nBC msimu uliomalizika
Timu zimepangwa katika makundi manne ya timu nne nne ambao timu mbili kutoka kila kundi zitafuzu robo fainali
Mechi ya ufunguzi ni kati ya Ruvu Shooting dhidi ya Namungo Fc leo saa 8 mchana na kufuatiwa na mechi nyingine kulingana na ratiba
Mtibwa Sugar ndio mabingwa wa michuano hiyo wakishinda kwa misimu minne mfululizo
