Baada ya tetesi nyingi kumuhusu kiungo mahiri wa Azam Fc, James Akaminko, jana klabu hiyo ilitangaza kumuongeza mkataba
Akaminko ameongeza mkataba wa miaka miwili ambao utakaomuweka klabuni hapo hadi 2026
Nyota huyo aliyen'gara katika kikosi cha Azam Fc msimu uliomalizika, alikuwa akihusishwa kuwindwa na matajiri wa Kariakoo klabu za Simba na Yanga
Anakuwa mchezaji wa pili kuongeza mkataba katika klabu ya Azam Fc baada ya Sospeter Bajana ambaye pia alikuwa akihusishwa na Simba