Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amesema klabu hiyo itamtangaza Kocha wake Mkuu baada ya Mkutano Mkuu wa Wanachama ambao utafanyika Jumamosi, Juni 24 jijini Dar es salaam
Kamwe amesema kocha atahusika na michakato yote ya usajili, hivyo baada ya kutambulishwa atafanya kazi na viongozi katika usajili
Aidha Kamwe amebainisha kuwa hatma ya kocha msaidizi Cedric Kaze na wengine katika benchi la ufundi itategemea na mapendekezo ya kocha wao mpya
"Baada ya Mkutano Mkuu tutamtangaza Kocha Mkuu, kisha tutaanza kutangaza Wachezaji wapya. Sisi sio kama zile klabu zingine, tutatambulisha kocha kisha Wachezaji ili aijenge timu yeye mwenyewe"
"Kuhusu Cedric Kaze, tutamuuliza kocha mpya, kama atakuwa na wasaidizi wake basi Cedric Kaze tutampangia kazi nyingine," alisema Kamwe
Kamwe pia amethibitisha klabu ya Yanga kuanza mazungumzo ya kumuongeza mkataba mshambuliaji wao kinara, Fiston Mayele
"Kwanza ieleweke, Mayele ni mchezaji wa Yanga ana mkataba wa mwaka mmoja, mazungumzo yakuboresha mkataba ni jambo la kawaida kwa klabu yetu pale mchezaji anapofanya vizuri"