Nyoni aibukia Namungo Fc

Joel JJ By Joel JJ β€’ 23rd June 2023


Nyoni aibukia Namungo Fc

Baada ya klabu ya Simba kutangaza kuachana na kiungo mkongwe Erasto Nyoni, ni rasmi mchezaji huyo kiraka ametua Namungo Fc amnbao wametambulisha usajili wake leo

"Tunayofuraha kuwataarifu kuwa Erasto Edward Nyoni amejiunga kuitumikia Timu yetu ya Namungo Fc akitokea Simba Sc. Karibu kwenye Familia ya Wauwaji wa Kusini Erasto Edward Nyoni," ilisema taarifa ya Namungo

Jana Simba ilitangaza kuachana na Nyoni baada ya kuwatumikia wekundu wa Msimbazi kwa miaka sita

Beno Kakolanya na Jonas Mkude nao waitangazwa kutokuwa sehemu ya kikosi cha Simba pia

Beno na Mkude wanatajwa kujiunga na klabu ya Singida Fountain Gate (zamani Singida Big Stars)


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.