Klabu ya Mashujaa ya Mkoani Kigoma imefanikiwa kupanda Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara 2023/2024 baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mbeya City katika mchezo wa marudiano wa Mchujo wa kuwania kucheza ligi hiyo msimu ujao uliofanyika jana kwenye Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya
Bao pekee la Mashujaa lilifungwa na John Budeba dakika ya 87 na kwa kwa matokeo hayo Mashujaa imepanda Ligi Kuu kwa ushindi wa jumla wa mabao 4-1 kufuatia ushindi mabao 3-1 katika mchezo wa kwanza uliofanyika kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika Mkoani Kigoma wiki iliyopita
Msimu ujao wa 2023/24 ligi kuu itakaribisha wageni watatu kutoka Championship, mbali na Mshujaa timu nyingine iliyoanda Ligi Kuu ya NBC msimu ujao ni Mabingwa wa Championship 2022/2023 JKT Tanzania na washindi wa pili, Kitayosce FC ya Tabora
ruvu Shooting, Polisi Tanzania na Mbeya City zitaalikwa huko Championship