Jana klabu ya Singida Fountain Gate ilitangaza kumuongeza mkataba kiungo raia wa Brazil, Bruno Gomez
Gomez amesaini mkataba wa miaka miwili kuendelea kuitumikia Singida Fountain Gate
Gomez alikuwa akihusishwa na klabu ya Simba ambayo ilianza mchakato wa kumsajili kabla ya matajiri ya Singida kushtuka na haraka kumfunga na mkataba mnono
Kiungo huyo anayeweza kucheza nafasi zote katika safu ya kiungo, alikuwa kinara wa mabao katika kikosi cha Singida BS akifunga mabao tisa
Alijumuishwa katika kikosi bora cha msimu ligi kuu ya NBC akiwa miongoni mwa waliowania tuzo ya kiungo bora