Simba - Yanga - Azam - Singida - Local

Bodi ya Ligi yateta na zinazoshiriki Kimataifa

Joel JJ By Joel JJ
β€’
26 Jun 2023
Bodi ya Ligi yateta na zinazoshiriki Kimataifa

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imekutana na Wakurugenzi Watendaji wa klabu nne zilizopata nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa ya CAF ili kupanga mikakati ya namna gani zijipange kuelekea msimu mpya wa mashindano yao

Timu hizo ambazo ni Yanga, Simba zitakazoshiriki Ligi ya Mabingwa Afrika, Azam FC na Singida Fountain Gate kwenye Kombe la Shirikisho Afrika pamoja na Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) 

Mabosi hao walikutana kuona namna gani ratiba yao ilivyo na kuwashauri jinsi ya kusajili vikosi vipana na kujiandaa vyema kutokana na namna miundombinu ilivyo nchini wanapokwenda kucheza mechi za ugenini

Afisa Mtendaji Mkuu wa TPLB, Almasi Kasongo alisema timu hizo zinatakiwa kujiandaa vizuri kwa mambo mawili, kiuchumi na usajili

"Miundombinu yetu sio rafiki sana, hivyo hawa wawakilishi wetu wanapaswa kujiaandaa vizuri sana kuanzia uchumi hadi usajili wao, wawe na vikosi vipana maana ratiba inaweza kuwabana, wakatoka kucheza nje ya nchi halafu wakifika hapa wanakuwa na mechi za nje ya mikoa yao"

"Hivyo kuna kila sababu ya kujipanga vizuri kwao kwneye mambo hayo mawili na tutajitahidi kutengeneza ratiba ambayo itakuwa rafiki kwa timu zote ili pia kuepukana na mechi za viporo," alisema Kasongo

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
4h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
4h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
4h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
8h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
11h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
12h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
12h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
13h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
14h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
15h ago
READ MORE β†’