Mbeya - Local

Kocha Mbeya City ajiuzulu

Joel JJ By Joel JJ
β€’
28 Jun 2023
Kocha Mbeya City ajiuzulu

Kocha wa Mbeya City Abdallah Mubiru amethibitisha kuachana na timu hiyo baada ya kushuka daraja, huku akitaja sababu mbili zilizochangia matokeo hayo

Mubiru alisaini kandarasi ya miaka miwili, ambapo kulikuwa na kipengele cha kuongeza mkataba iwapo watabaki ligi kuu na kuvunjika kama timu itashuka daraja na matokeo ndivyo kama ulivyosikia na kuona

Mbeya City ilishuka daraja kupitia play off baada ya kufungwa jumla ya mabao 4-1 dhidi ya Mashujaa ya Championship na kuungana na Polisi Tanzania na Ruvu Shooting zilizoshuka mapema baada ya kumaliza ligi nafasi mbili za mwisho

Mubiru raia wa Uganda alisema kutokana na mkataba ulivyokuwa kwa sasa yuko huru, huku akieleza kuwa sababu ya kushuka timu hiyo ni kikosi dhaifu na kwamba alikosa watu aliohitaji akiwamo kipa, beki wa kushoto na straika baada ya Paul Nonga kustaafu

Pia alisema City ilifanyiwa hujuma za wazi kuanzia mchezo dhidi ya Yanga, KMC na zile za play off (mtoano) na Mashujaa hali ambayo iliwapa wakati mgumu na kwamba kwa sasa anaenda kwao kupumzika kusubiri ofa mpya popote

"Hata angekuwa Pep Guadiola kwa kikosi changu asingetoboa, wachezaji hawakuwa na kiwango, lakini niliomba kupata kipa, beki wa kushoto na straika wa kusaidiana na Tariq Seif sikupata. Tulidhulumiwa pia baadhi ya mechi," alisema Mubiru

Kocha huyo alisema wakati anaenda mapumziko hakufurahishwa na tukio la kupigwa ngumi na mmoja wa viongozi wa benchi la ufundi la Mashujaa na kwamba haelewi dhamira ilikuwa ni nini

Alisema anashukuru kwa sasa hali yake inaendelea vyema baada ya matibabu hospitali akibainisha kuwa kiongozi huyo alimtafuta mara ya kwanza akamkwepa kabla ya kumrudia tena na kumpiga

"Mimi simjui na dhamira yake sielewi ilikuwa nini. Alianza kunitafuta nikamkwepa mara ya kwanza, lakini alirudi akanipiga akavunja miwani ikanijeruhi na nimetoka hospitali naendelea vizuri," alisema kocha huyo asiye na maneno mengi

Mwenyekiti wa Mbeya City, Joseph Mlundi alisema wanasubiri kikao cha viongozi wa mkoa ili kujadili tathmini ya ligi kwa ujumla na maazimio na kuja na tamko la kulaani tukio la kocha kupigwa

"Kujua tutabaki na kocha au kuachana naye haijajulikana tunasubiri kikao cha uongozi wa juu, lakini nadhani tutakuja na taarifa rasmi la kulaani tukio hilo ambalo si la kiungwana," alisema Mlundi

Mwanaspoti

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
1h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
1h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
2h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
5h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
8h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
9h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
10h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
10h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
11h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
12h ago
READ MORE β†’