Transfer - International

Tetesi za soka Ulaya, Ijumaa Juni 30 2023

Joel JJ By Joel JJ
β€’
30 Jun 2023
Tetesi za soka Ulaya, Ijumaa Juni 30 2023

Beki wa Uholanzi Jurrien Timber, 22, anatazamiwa kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu na Arsenal baada ya kukubaliana ada ya awali ya euro 42m (£36.2m) na Ajax. (De Telegraaf – In Deutsch)

Aston Villa wamekubali mkataba wa pauni milioni 35 kumsajili beki wa Uhispania Pau Torres, 26, kutoka Villarreal. (Guardian)

West Ham bado wanasubiri Arsenal kuwasilisha mpango wa malipo unaokubalika kwa ununuzi wa pauni milioni 105 wa kiungo wa kati wa Uingereza Declan Rice, 24. (Sun)

Chelsea wanashinikiza kufikia makubaliano na Brighton kuhusu usajili wa Moises Caicedo, huku kiungo huyo wa kati wa Ecuador, 21, akiwa tayari amekubali masharti ya kibinafsi. (Fabrizio Romano)

Beki wa Bayern Munich na Ufaransa Lucas Hernandez, 27, yuko mbioni kuhamia Paris St-Germain. (Fabrizio Romano)

Kiungo wa kati wa Celta Vigo Mhispania Gabri Veiga, 21, ametambuliwa na Chelsea kama mbadala bora wa kiungo wa kati wa Uingereza anayekwenda Manchester United Mason Mount, 24. (Standard)

Aston Villa wanafikiria kumnunua kwa mkopo winga wa Barcelona na Uhispania Ferran Torres, 23, na chaguo la kumnunua la euro 25m (£21.5m). (Mundo Deportivo – In Spanish)

Kiungo wa kati wa zamani wa Uingereza Ruben Loftus-Cheek, 27, yuko nchini Italia kukamilisha uhamisho wa kudumu kutoka Chelsea hadi AC Milan, ambaye baadaye atamlenga winga wa Chelsea wa Marekani Christian Pulisic, 24. (Standard)

Mshambulizi wa Chelsea na Ubelgiji Romelu Lukaku, 30, amekataa ofa ya pili kutoka kwa klabu ya Saudi Arabia Al-Hilal - yenye thamani ya £45m (£39m) kwa mwaka - kwani anataka tu kuondoka kwenda Inter Milan. (Gazzetta dello Sport – in Itali)

Juventus, Borussia Dortmund na Bayer Leverkusen wanavutiwa na mshambuliaji wa Sheffield United wa England chini ya miaka 20 Daniel Jebbison, 19. (90min)

Manchester United na Chelsea zote zinamtaka mlinda mlango wa Aston Villa kutoka Argentina Emiliano Martinez, 30. (Football Transfers)

Meneja wa Manchester United Erik ten Hag amemzuia mlinda mlango wa Uingereza Tom Heaton, 37, kuhamia Luton Town, huku kukiwa na hali ya sintofahamu kuhusu mustakabali wa mlinda mlango wa Uhispania David de Gea, 32. (Telegraph – Subscription Required)

Wilfried Zaha atakuwa mchezaji huru siku ya Ijumaa, lakini fowadi huyo wa Ivory Coast, 30, bado yuko kwenye mazungumzo na Crystal Palace ili akubali mkataba mpya. (Mail)

Beki wa kushoto wa Arsenal Mreno Nuno Tavares, 23, anawindwa na West Ham. (iNews – Subscription Required)

Arsenal wamefaulu kumshawishi kiungo wa kati wa Uingereza Ethan Nwaneri, 16, kukabidhi mustakabali wake katika klabu hiyo, licha ya Chelsea na Manchester City kumtaka. (Telegraph – Subscription Required)

Meneja wa Roma Jose Mourinho anatazamia kumnunua mshambuliaji wa Leicester City wa Nigeria Kelechi Iheanacho, 26, na fowadi wa Zambia Patson Daka, 24. (Express)

Mshambulizi wa zamani wa Leicester Uingereza Jamie Vardy, 36, amekataa nia ya klabu ya Saudi Arabia Khaleej FC. (Guardian)

Daniel Farke yuko mbioni kuwa meneja mpya wa Leeds United, huku klabu hiyo ikitarajia kuwa na Mjerumani huyo, 46, kwa ajili ya kuanza mazoezi ya kujiandaa na msimu ujao wiki ijayo. (Mail)

Aliyekuwa meneja wa Crystal Palace Patrick Vieira, 47, ameonekana kupendekezwa kuwa meneja wa klabu ya Ligue 1 ya Strasbourg. (Mail)

BBC

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
4h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
4h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
4h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
8h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
11h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
12h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
12h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
13h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
14h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
15h ago
READ MORE β†’