Kwa mujibu wa Afisa habari wa klabu ya KMC Mwanadada Christina Mwagala amesema uongozi wa timu hiyo metenga bajeti ya Usajili inayofikia Bilioni 1 za kitanzania
Mwagala amesema malengo yao kwa msimu ujao ni kutwaa ubingwa Ligi Kuu ya NBC
Mwagala ametamba kuwa hawatasajili wachezaji walioachwa kutoka kwenye vilabu vya Simba,Yanga na Azam
Amesema watasajili wachezaji wapya na bora zaidi kuelekea kwenye dirisha kubwa hili la Usajili
KMC iliponea chupuchupu ikisalia ligi kuu baada ya kushinda mchezo wa play-off dhidi ya Mbeya City ambayo imeshuka daraja