Ligi Kuu ya Vijana U20 ilifikia tamati jana usiku ambapo Mtibwa Sugar ilifanikiwa kutwaa ubingwa baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Geita Gold
Ni katika mchezo wa fainali ya michuano hiyo ambayo ilipigwa katika uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar es salaam
Huo ni msimu wa tano mfululizo Mtibwa Sugar wanashinda taji la mashindano hayo yanayohusisha timu za vijana wa U20 kwa klabu zote zinazoshiriki ligi kuu
Unaweza kusema Mtibwa Sugar sasa ni mabingwa wa kihistoria wa mashindano hayo
Azam Fc ilimaliza nafasi ya tatu baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo uliopigwa mapema