Afisa Mtendaji Mkuu wa Geita Gold Fc Simon Shija amesema timu hiyo inatarajiwa kufanya maboresho makubwa katika dirisha hili ya usajili
Geita Gold ilimaliza nafasi ya saba katika msimamo wa ligi 2022/23 timu hiyo ikiwa imeshuka kwa nafasi tatu kutoka nafasi ya nne waliyomaliza msimu wa 2021/22
Shija amesema mpaka sasa wamewakabidhi wachezaji saba barua za kuachana nao lakini pia wapo wengine wataachwa
"Kwa sasa tumewapa barua wachezaji saba lakini wengine watatu bado tunaendelea kuongea nao tena na kama tutashindwana basi nao tutawafungulia mlango wa kutokea japo hatutamani hilo kutokea"
Shija aliongeza moja ya mchezaji waliopo kwenye mazungumzo ya mkataba mpya ni Elias Maguri ambaye wanatamani kuendelea naye msimu ujao baada ya kuonyesha kiwango kizuri tangu ajiunge nao
Wachezaji waliopewa ‘Thank You’ ni; Fabrice Kayemba, Arakaza MacArthur, Shown Oduro, Mussa Gadi, Jeremiah Thomas na mchezaji raia wa Japan



