Transfer - International

Tetesi za soka Ulaya, Alhamisi Julai 06 2023

Joel JJ By Joel JJ
6 Jul 2023
Tetesi za soka Ulaya, Alhamisi Julai 06 2023

Tottenham wamempa mshambuliaji wa Uingereza Harry Kane, 29, ofa ambayo itaboresha sana mshahara wake wa sasa wa pauni laki 2kwa wiki akiamua kubaki katika klabu hiyo. (Guadian)

Kocha wa Bayern Munich Thomas Tuchel amekutana na Kane nyumbani kwake huku klabu hiyo ya Ujerumani ikijaribu kumsajili mchezaji huyo. (Bild, via Mail)

AC Milan wamewasilisha ofa iliyoboreshwa ya pauni milioni 24 kwa ajili ya winga wa Chelsea na Marekani Christian Pulisic, 24. (Mail)

Manchester United wanatayarisha dau la pauni milioni 39 kwa ajili ya mlinda mlango wa Inter Milan raia wa Cameroon Andre Onana, 27. (Fabrizio Romano)

Arsenal wamefikia mkataba wa £38.5m na Ajax kwa ajili ya beki wa Uholanzi Jurrien Timber, 22. (Standard)

The Gunners watatumia hadi karibu pauni milioni 200 ya bajeti yao ya majira ya joto baada ya kuafikiana na Timber na kiungo wa kati wa West Ham wa Uingereza Declan Rice, 24. (Telegraph)

Newcastle wanaongoza katika kinyang'anyiro cha kumnunua kiungo wa kati wa Leicester City na Uingereza Harvey Barnes, 25, huku Aston Villa na Tottenham pia zikiwania. (Guadian)

Chelsea wanatayarisha ofa ya pauni milioni milioni 85 kwa kiungo wa kati wa Brighton wa Ecuador Moises Caicedo, 21. (Diego Arcos, via Football.London)

The Blues pia wanavutiwa na kiungo wa kati wa Southampton raia wa Ubelgiji Romeo Lavia, 19. (Sky Sports)

Mchezaji mpya wa Manchester United Mason Mount, 24, alikataa ofa ya £200k kwa wiki kutoka kwa Chelsea kujaribu kumbakisha kiungo huyo wa kati wa Uingereza Stamford Bridge mwezi Februari. (Athletic - Usajili unahitajika)

Aston Villa na Everton ni miongoni mwa klabu za Ligi Kuu ya Uingereza zinazomtaka mshambulizi wa Leeds United na Italia Wilfried Gnonto, 19. (Football Insider)

Liverpool bado wanavutiwa na beki wa Uingereza Levi Colwill, 20, ambaye Chelsea bado wanahitaji huduma zake. (Football.London)

BBC

More Stories

Wamebaki wababe wawili tu wasiofungika Ligi Kuu
Wamebaki wababe wawili tu wasiofungika Ligi Kuu
13h ago
READ MORE →
Afcon haiwezi kuondoka Tanzania, Kenya na Uganda : Motsepe
Afcon haiwezi kuondoka Tanzania, Kenya na Uganda : Motsepe
14h ago
READ MORE →
BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
16h ago
READ MORE →
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
16h ago
READ MORE →
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
17h ago
READ MORE →
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
17h ago
READ MORE →
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
17h ago
READ MORE →
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
18h ago
READ MORE →
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa  Yanga SC “Your next: Yanga”
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa Yanga SC “Your next: Yanga”
18h ago
READ MORE →
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
20h ago
READ MORE →