Diao aiponza Azam Fc

Joel JJ By Joel JJ β€’ 7th July 2023


Diao aiponza Azam Fc

Baada ya Azam Fc kumtangaza mshambuliaji Alassane Diao raia wa Senegal kutoka klabu ya US Goree, miamba hiyo ya Senegal imesikitishwa na kitendo cha Waoka Mikate hao kumsajili nyota wao huyo ambaye bado ana mkataba nao

Kupitia taarifa yake kwenye mitandao ya kijamii klabu hiyo ambaye Rais wake ndio Rais wa Shirikisho la Soka la Senegal, Augustin Senghor imebainisha kuwa Alassane Diao bado ana mkataba na US Goree na inaashiria kuwa hakuna mazungumzo yoyote ambayo yaliyoanzishwa na Azam FC juu ya mchezaji huyo

"Kupitia mitandao ya kijamii, UNION SPORTIVE GOREENNE imebaini kuhusu utiaji saini wa mkataba wa miaka miwili kati ya mchezaji wetu ALASSANE DIAO na klabu ya AZAM FC ya TANZANIA"

"Mchezaji ALASSANE DIAO bado ana mkataba na US Goree, na kwamba hakuna mazungumzo yoyote yaliyoanzishwa na klabu ya AZAM FC (TANZANIA) katika mwelekeo wa kumwachilia mchezaji huyo hivyo hawezi kufuzu kucheza katika klabu nyingine nchini Senegal au kimataifa kabla ya mwisho wa mkataba wake wa sasa"

"Kwa kuheshimu taratibu zinayosimamia soka, US Goree inasisitiza dhamira yake ya kutii sheria za uhamisho zilizowekwa na FIFA na kuhakikisha maslahi ya klabu na wachezaji wake walio chini ya mkataba" imesema taarifa hiyo


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.