Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amewasili nchini usiku wa kuamkia leo akitokea Hispania
Ujio wa kocha huyo ni ishara sasa Yanga iko tayari kuanza maandalizi ya msimu mpya ambapo siku ya Jumatatu atawakaribisha wachezaji wake Avic Town
Aidha wakati wowote Yanga itatangaza benchi la ufundi kabla na kuanza zoezi la kutangaza wachezaji wapya, zoezi linalosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa Yanga
Yanga ilimpa Gamondi nafasi ya kuamua watu ambao atafanya nao kazi katika benchi la ufundi hivyo Wananchi watarajie kuona mabadiliko
Nafasi zinazosubiriwa kutangazwa ni Kocha Msaidizi, Kocha wa magolikipa, Kocha wa viungo na mchambuzi wa sayansi ya mpira (Football Analyst)