Yanga yapokea Milioni 405 bonas SportPesa

Joel JJ By Joel JJ β€’ 10th July 2023


Yanga yapokea Milioni 405 bonas SportPesa

Klabu ya Yanga imekabidhiwa bonas ya Tsh Milioni 405 na kampuni ya SportPesa baada ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC, Kombe la FA na Ngao ya Jamii

Bonas hiyo ni sehemu ya makubaliano ya mkataba wa Udhamini ambao bonas hiyo inatolewa pale Yanga inapotwaa ubingwa au inapofanya vizuri katika michuano ya Kimataifa

"Tunawapongeza Yanga kwa mafanikio waliyopata msimu uliopita. Sisi tunajivunia kuwa Wadhamini wao kwani wametutangaza vizuri"

"Leo tunajisikia fahari kuikabidhi Yanga Tsh Milioni 405 kama asante kwa mafanikio makubwa waliyopata msimu uliopita ambao walishinda mataji yote"

"Naamini kwa kuangalia mipango yao, msimu huu wanaweza kupata mafanikio makubwa zaidi," alisema Abbas Tarimba Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya SportPesa


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.