Simba - Local - Transfer

Simba yazima tetesi kuhusu Chama

Joel JJ By Joel JJ
β€’
14 Jul 2023
Simba yazima tetesi kuhusu Chama

Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ally 'amewakata maini' wale wanaodhani Simba ina mpango wa kuachana na kiungo wake kinara wa pasi za mwisho Clatous Chama 'Mwamba wa Lusaka'

Ahmed amesema Chama ambaye bado ana mkataba wa mwaka mmoja na Simba yuko kwenye mipango ya Wekundu hao wa Msimbazi wala hakuna ofa iliyowasilishwa mezani kumtaka

Ahmed amewataka Wanasimba wapuuze taarifa zinazosambazwa huko kwenye mitandao ya kijamii kuhusu Chama kwani yupo sana

"Iko hivi, Chama bado ana mkataba na Simba kwa muda wa mwaka mmoja hadi Juni 30 2024. Hatujapokea ofa kutoka klabu yeyote ikihitaji kumnunua Chama na wala hatujapokea maombi ya mchezaji kutaka kuvunja mkataba"

"Mchezaji yeyote ambae tunamhitaji atabaki kuitumikia Simba kulingana na mahitaji ya mkataba wetu," alisema Ahmed

Chama anatarajiwa kuungana na wenzake katika pre-season huko Uturuki ambapo Ahmed amesema msafara wa pili utawasili Uturuki Jumatatu ukijumuishwa wachezaji wote waliobaki jijini Dar es salaam kutokana na sababu mbalimbali

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
7h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
7h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
7h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
11h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
14h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
15h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
15h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
16h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
17h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
18h ago
READ MORE β†’