Ni rasmi klabu ya Simba imetambulisha usajili wa kiungo mahiri Fabrice Ngoma kutoka klabu ya Al Hilal ya Sudan
Huu unaweza kuwa usajili mkubwa zaidi uliofanywa katika dirisha hili la usajili mpaka sasa
Ngoma ni mchezaji wa daraja la juu ambaye amepata mafanikio katika klabu alizopita
Baada ya kupata mafanikio makubwa akiwa na AS Vita, msimu wa 2018/19 Ngoma akajiunga na Raja Casablanca kwa misimu mitatu kabla ya kutimkia Arabuni alikocheza kwa muda mfupi kisha kurejea Afrika alikojiunga na Al Hilal msimu uliopita
Aliitumikia Al Hilal kwa msimu mmoja tu ambapo hivi karibuni alivunja mkataba wake wa miaka miwili uliokuwa umesalia na timu hiyo
Inafahamika huko Sudan hakuna mazingira rafiki ya kucheza soka kutokana na vita inayoendelea, hii ndio sababu iliyopelekea Ngoma kuvunja mkataba wake sambamba na wachezaji wengine watatu



