West Ham wanampango wa kumsajili beki wa kati wa England Harry Maguire, 30, kwa mkopo kutoka Manchester United. (Athletic)
Kiungo wa kati wa Uholanzi Frenkie de Jong, 26, anaweza kupelekwa Manchester City kama sehemu ya mpango wa kubadilishana utakaomhusisha Mreno Bernardo Silva, 28, kwenda Barcelona. (Mirror)
Mtendaji mkuu wa Bayern Munich Uli Hoeness anaamini kwamba mshambuliaji wa Tottenham Hotspur na England Harry Kane, 29, atahamia Ujerumani msimu huu wa joto. (kicker)
Huku kukiwa na sintofahamu ya mustakabali wa Kane, Tottenham Hotspur inafuatilia kumnunua mshambuliaji wa Juventus na Serbia Dusan Vlahovic mwenye umri wa miaka 22. (Rudy Galetti)
Newcastle United wameripotiwa kuweka mezani dau la pauni milioni 82 kumnunua winga wa Napoli mwenye umri wa miaka 22 wa Georgia Khvicha Kvaratskhelia. (Express)
Wolves wanatazamiwa kuwasilisha ofa ya thamani ya zaidi ya pauni milioni 20 kumnunua kiungo wa kati wa Bristol City na England Alex Scott, 19. (Telegraph)
Kiungo wa kati wa Liverpool na Brazil Fabinho, 29, ameachwa kwenye kambi yao ya kujiandaa na msimu mpya nchini Ujerumani kutokana na ofa ya pauni milioni 40 kutoka kwa klabu ya Saudi Arabia Al-Ittihad. (Daily Star)
Nahodha wa Liverpool, Jordan Henderson amekubali maslahi binafsi na klabu ya Al Ettifaq lakini bado hakuna makubaliano kati ya vilabu hivyo viwili. (Fabrizio Romano)
Pierre-Emerick Aubameyang yuko tayari kuondoka Chelsea kwenda Marseille, huku mshambuliaji huyo wa Gabon akiwa tayari kupunguza mshahara wake kufanikisha uhamisho huo. (GOAL)
Beki wa kati Jonny Evans, 35, ambaye yuko huru, anasakwa na bosi wake wa zamani Brendan Rodgers kwa ajili ya kuhamia Celtic. Wawili hao raia wa Ireland Kaskazini wamefanya kazi pamoja Leicester City. (Sun)
Leicester City wanamtaka kiungo wa kati wa Italia Cesare Casadei, 20, kwa mkopo kutoka Chelsea. (Mail) Winga wa Algeria Riyad Mahrez, 32, anaendelea kuwa mada ya majadiliano kati ya Manchester City na Al Ahli ya Saudi Arabia. (Fabrizio Romano)
Winga wa Newcastle mwenye umri wa miaka 26 Mfaransa Allan Saint-Maximin, pia anasakwa na waarabu wa Al Ahli. (Alkass) Mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku, 30, hatajiunga na Inter Milan baada ya timu hiyo ya Italia kuachana na mpango wake huo, huku Saudi Arabia au klabu nyingine ya Serie A Juventus vikimvutia mshambuliaji huyo wa Chelsea. (Fabrizio Romano)
Kiungo wa kati wa Nottingham Forest Jonjo Shelvey, 31, anakaribia kuondoka The City Ground, baada ya kiungo huyo wa kati wa Uingereza kuachwa nje ya kambi yao ya kujiandaa na msimu mpya. (Athletic)
Sheffield United iliyopanda daraja hivi karibuni inafikiria kumnunua Shelvey. (Mirror) Juventus wanasaka saini ya kiungo wa kati wa Barcelona na Ivory Coast Franck Kessie, 26. (Fabrizio Romano)
Kiungo wa kati wa zamani wa Leicester City Danny Drinkwater, 33, anasema angependa kurejea The Foxes, miaka sita baada ya kuhamia Chelsea. (Mirror)
BBC