Tetesi za usajili Ulaya, Jumatatu, Julai 17 2023

Joel JJ By Joel JJ β€’ 17th July 2023


Tetesi za usajili Ulaya, Jumatatu, Julai 17 2023

Liverpool wanatazamia kumnunua kiungo wa Manchester City na Uingereza Kalvin Phillips, 27, wakati Fabinho anakaribia kuhamia Saudi Arabia. (Mirror)

West Ham wako kwenye mazungumzo ya kumsajili kiungo wa Ureno Joao Palhinha, 27, kutoka Fulham. (Talksport)

Erik ten Hag yuko tayari kumuuza kiungo wa kati wa Manchester United na Scotland Scott McTominay, 25, ili kufadhili uhamisho wa majira ya joto. (Metro)

Baada ya kujiondoa kwenye kinyang'anyiro cha kumnasa mshambuliaji wa Chelsea na Ubelgiji Romelu Lukaku, 30, Inter Milan wameelekeza macho yao kwa mshambuliaji wa Atletico Madrid mwenye umri wa miaka 30 Alvaro Morata na mshambuliaji wa Arsenal mwenye umri wa miaka 22 Folarin Balogun. (La Gazzetta - kwa Kiitaliano)

Lukaku hatasafiri katika ziara ya Chelsea ya kujiandaa na msimu mpya, huku kipaumbele chake kikiwa ni kumuuza kwa £34m.

Usajili wa Juventus unategemea mkataba kati ya mshambuliaji wa Paris St-Germain na Mserbia Dusan Vlahovic, 23. (Fabrizio Romano)

Kipa wa zamani wa Manchester United David de Gea, 32, anatarajiwa kuhamia Saudi Arabia baada ya mlinda mlango huyo wa zamani wa Uhispania kupokea ofa nyingi kutoka kwa zaidi ya klabu moja. (Daily Star)

Kiungo wa kati wa Argentina Giovani lo Celso, 27, anakaribia kuondoka Tottenham Hotspur huku Napoli wakianzisha mazungumzo kwa ajili ya mchezaji huyo. (Daily Mail)

Nottingham Forest wana nia ya kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa Brazil Matheus Nascimento mwenye umri wa miaka 19 kutoka Botafogo. (UOL - kwa Kireno)

Licha ya West Ham kuinyesha nia ya kutaka kumnunua beki wa Ujerumani Jonathan Tah, 27, mchezaji hiyo anatazamia kusalia katika klabu ya Bundesliga Bayer Leverkusen. (Kicker - kwa Kijerumani)

Leicester City na Burnley wanatazamia kukutana ana kwa ana katika mpango wa kumsajili kwa mkopo kiungo mshambuliaji Cole Palmer, 21, kutoka Manchester City. (Leicestershire Live)

Beki wa Ivory Coast Eric Bailly, 29, na mlinzi wa Brazil Alex Telles, 30, walishindwa kufika siku ya kwanza ya mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya wa Manchester United huku kukiwa na mipango ya kuuzwa. (Mirror)

BBC


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.