Aliyekuwa kocha wa Yanga, Masreddine Nabi amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu ya FAR Rabat ya Morocco
Nabi anatua kwa mabingwa hao wa Ligi Kuu ya Morocco baada ya mafanikio makubwa aliyopata wakati akiwa na klabu ya Yanga
Nabi aliiongoza Yanga kushinda mataji sita katika misimu miwili pamoja na kutinga fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika (CAF CC)
Alitangaza kuondoka mwishoni mwa msimu uliopita baada ya mkataba wake na Yanga kumalizika