Klabu ya Yanga imemsajili nyota wa Marumo Gallants, Mahlatse Makudubela 'Skudu' kwa mkataba wa mwaka mmoja
Winga huyo anayetumia hasa mguu wa kushoto alikuwa miongoni mwa wachezaji muhimu walioifikisha Marumo hatua ya Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu uliopita ambayo walipoteza dhidi ya Yanga kwa kichjapo cha mabao 4-1 katika mechi mbili baina yao.
Yanga ilimtambulisha mchezaji huyo saa 6 usiku na kumkabidhi jezi namba sita ambayo viongozi wa Yanga waliinadi kwa takribani mwezi mmoja
Winga huyo anaweka rekodi ndani ya Yanga ya kuwa mchezaji wa kwanza raia wa Afrika Kusini kuwatumikia mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu ya NBC na Kombe la Shirikisho la Azam
Usajili huo unaifanya Yanga hadi sasa kufikisha idadi ya wachezaji watano wapya iliowanasa katika dirisha hili kubwa la usajili. Yanga tayari imeshawasainisha mabeki Nickson Kibabage, Gift Fred, kiungo Jonas Mkude, winga wa kulia Maxi Nzengeli na sasa Skudu