Tetesi za soka Ulaya, Alhamisi Julai 20 2023

Joel JJ By Joel JJ
β€’
20 Jul 2023
Tetesi za soka Ulaya, Alhamisi Julai 20 2023

Chelsea wanafanyia kazi ofa iliyoboreshwa ya pauni milioni 80 pamoja na nyongeza kwa kiungo wa Brighton na Ecuador Moises Caicedo, 21. (Mail)

Chelsea pia wanafikiria kumrejesha Marc Guehi, miaka miwili baada ya kumuuza beki huyo wa Uingereza, 23, kwa Crystal Palace. (Guardian)

Manchester City wanamtaka winga wa Barcelona wa Brazil Raphinha, 26, kuchukua nafasi ya winga wao anayekwenda Al-Ahli kutoka Algeria Riyad Mahrez, 32. (Foot Mercato - kwa Kifaransa)

Newcastle wanakaribia kumuuza winga Mfaransa Allan Saint-Maximin, 26, kwa klabu ya Saudi Arabia Al-Ahli kwa takriban pauni milioni 30. (Telegraph - usajili unahitajika)

Al-Nassr wameboresha dau lao la kumnunua Moussa Diaby wa Bayer Leverkusen, huku Aston Villa wakiwasilisha ombi la pili kwa winga huyo wa Ufaransa, 24. (Fabrizio Romano).

Crystal Palace inatarajiwa kuweka thamani ya kima cha chini cha pauni milioni 70 kwa kiungo wa kati wa Mali Cheick Doucoure, 23, ambaye ananyatiwa na Liverpool. (Mail)

ottenham wanafikiria kumnunua mshambuliaji wa Brazil Pedro, 26, anayechezea Flamengo. (Independent)

Dau la pauni milioni 15 linaweza kutosha kwa Bournemouth kushinda vilabu vya Borussia Dortmund, Barcelona na Real Madrid katika usajili wa beki wa Uhispania Ivan Fresneda, 18, kutoka Real Valladolid msimu huu. (Football Insider)

Fulham wametoa ofa ya awali ya £15m kwa Ajax kumnunua beki wa Nigeria Calvin Bassey, 23. (Athletic -Usajili unahitajika)

Mshambulizi wa Serbia Aleksandar Mitrovic, 28, amesema hatawahi kuichezea Fulham tena baada ya kukataa ofa mbili kutoka kwa Al-Hilal. (Sky Sports)

Atletico Madrid wamempa mshambuliaji wa Ureno Joao Felix, 23, idhini ya kukamilisha uhamisho wake kwenda Barcelona. (AS - kwa Kihispania)

Atletico wamewasiliana na Paris St-Germain kuhusu upatikanaji wa Marco Verratti lakini bado hawajatuma ofa kwa kiungo huyo wa kati wa Italia, 30. (L'Equipe - kwa Kifaransa)

Chelsea huenda wakakamilisha uhamisho wa Elye Wahi wa Montpellier lakini Atletico Madrid pia wanamwania mshambuliaji huyo wa Ufaransa, 20. (L'Equipe - in French)

Tottenham wameungana na West Ham katika kinyang'anyiro cha kumnunua Conor Gallagher msimu huu wa joto kutoka Chelsea, ambao wanaaminika kushikilia ada ya angalau £40m kwa kiungo huyo wa kati wa Uingereza, 23. (Football Insider)

Arsenal wanamfuatilia kiungo wa Dinamo Zagreb Martin Baturina, 20, ambaye aliivutia Croatia kwenye michuano ya Uropa ya Vijana chini ya miaka 21. (Express)

Villarreal wana nia ya kumsajili beki wa Ureno Cedric Soares, 31, kutoka Arsenal. (Sport - kwa Kihispania)

Real Betis wanavutiwa na kiungo wa kati wa West Ham na Uhispania Pablo Fornals, 27, pamoja na kiungo wa kati wa Tottenham na Argentina Giovani lo Celso, 27. (Relevo - kwa Kihispania)

Tottenham wamempa beki wa Colombia Davinson Sanchez, 27, ruhusa ya kufanya mazungumzo na Strasbourg na Spartak Moscow. (Dakika 90)

Wolves wako kwenye mazungumzo ya kumsajili beki wa zamani wa Uingereza Aaron Cresswell, 33, kutoka West Ham. ( Athletic -Usajili unahitajika)

Napoli na Torino wako mbioni kumsajili kiungo wa kati Mfaransa Boubakary Soumare, 24, kutoka Leicester. (L'Equipe - kwa Kifaransa)

BBC

ADVERTISE HERE

More Stories

De Klassiker hakuna mshindi, Bayern 2-2 Dortmund
De Klassiker hakuna mshindi, Bayern 2-2 Dortmund
9h ago
READ MORE β†’
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
11h ago
READ MORE β†’
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
11h ago
READ MORE β†’
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
12h ago
READ MORE β†’
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
12h ago
READ MORE β†’
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
13h ago
READ MORE β†’
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
16h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
18h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
19h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
19h ago
READ MORE β†’