Winga wa Yanga Mahlatse Makudubela 'Skudu' amewaalika mashabiki wa soka nchini kujitokeza kwa wingi uwanja wa Benjamin Mkapa kushuhudia mtanange wa kilele cha wiki ya Mwananchi dhidi ya Kaizer Chiefs ambao utapigwa kesho Jumamosi
Akizungumza katika mkutano na Wanahabari kuelekea mchezo huo, Skudu amesema wamewaandalia mashabiki burudani kubwa wanachopaswa kufanya ni kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa
"Tupo kwenye maandalizi ya awali kujiandaa na msimu mpya, kwa niaba ya wachezaji wenzangu kwanza niseme ni heshima kubwa sana kwangu kuwaalilisha kwenye mkutano huu na ujumbe wetu kwenu tunaomba kesho mje kwa wingi tumewaandalia burudani nzuri," alisema
Skudu ndiye mchezaji aliyekabidhiwa jezi namba sita ambayo kwa takribani mwezi mmoja ilinadiwa na viongozi wa Yanga
Amesema kukabidhiwa jezi hiyo ni heshima kubwa kwake, na atahakikisha anailinda thamani yake



